Thursday, November 26, 2015

Top banner

Top2

LOGO

Top logo

Top Ads

Habari afya

Habari afya (56)

Dar es Salaam, Tanzania. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepatiwa msaada wa vifaa kumi  vya tiba vya kuwahudumia watoto  mara wapougua na kufikishwa kwenye hospitali hiyo.

Vifaa hivyo vina thamani ya Dola za Kimarekani Laki moja sawa na zaidi Sh milioni 2 vimetolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF),kwa lengo la kupunguza vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

Baadhi ya vifaa vilivyotolewa  ni Ventilator, medical, adult –child ,w/access pamoja na Warmer system , newborn, radiant, w/access.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo  Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Dk Jama Gulaid amesema mchango wa UNICEF na michango ya wadau wengine itawezesha watumishi wa hospitali ya Muhimbili kuokoa maisha ya  watoto  ambao wanahitaji huduma za afya.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando  amesema  hadi kufikia mwaka 2013  Tanzania imefanikiwa kupunguza vifo vya watoto hao kwa theluthi mbili.

Kwa mujibu wa Dk Mmbando, mwaka 2013 Tanzania imepunguza vifo hivyo na kufikia 54 kwa vizazi hai 1,000  na kufikia lengo la Milenia  na kwamba  mafanikio hayo yametokana na kiwango kikubwa cha chanjo , matumizi sahihi  ya dawa za Malaria pamoja na vyandarua.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Mseru amewashukuru UNICEF kwa msaada huo ambao utachangia kwa kiasi kikubwa kuokoa maisha ya watoto na kuboresha huduma za afya.

Dar es Salaam, Tanzania: Katibu Mkuu Kiongozi wa IKULU, Balozi Ombeni Sefue amesema kwamba amefuatilia maagizo yalioagizwa na Rais John Pombe Magufuli aliyetembelea hospitali hiyo hivi karibuni. "Nimekagua mashine za MRI na CT SCAN na nimeambiwa kwamba zitakabilika alhamisi wiki hii (ndani ya siku tatu).

Balozi Ombeni Sefue.Dar es Salaam, Tanzania. Taarifa za ndani kutoka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) zinaeleza kwamba wafanyakazi wa hospitali hiyo wanafanyakazi hadi siku za wiki end hasa baada ya Rais John Magufuli kutembelea hospitali hiyo. Baadhi ya wafanyakazi ambao walikuwa hawaendi kazini Jumamosi na Jumapili hivi sasa wanakwenda kazini. Madaktari na manese wamekuwa wakienda kazini siku zote kwa kupangiana zamu.

Katika hatua nyingine, Leo Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue atatembelea hospitali hiyo kuona shughuli mbalimbali ikiwamo utekelezaji wa ahadi ya Rais Magufuli ya upatikanaji bora wa huduma na wapo wa vifaa vya kutosha kwa ajili ya wagonjwa.

Dar es Salaam, Tanzania. Agizo la Rais John Magufuli la kutaka Sh 200 milioni zitumike kwa ajili ya kununu vitanda kwa ajili ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) limetekelezwa mara moja LEO. Vitanda, magodoro na shuka  500 vimenunuliwa na vyote kupewa Taasisi ya Moi ambayo ipo Muhimbili. 

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

HOTUBA YA MKURUGENZI MTENDAJI KILELE CHA MAAZIMISHO YA SIKU YA WATOTO WALIZOZALIWA KABLA YA SIKU (NJITI) ILIYOSOMWA NOVEMBA 17, 2015

 

MGENI RASMI, MKUUWA MKOA WA DAR ES SALAAM, MHE SAID M SADICK,

MWANZILISHI WA TANZANIA PREMATURE FOUNDATION, BI DORIS MOLLEL 

Wapendwa Akina Mama na Watoto Wenu

Madaktari na Wauguzi

Waandishi wa Habari

Wageni Waalikwa

Mabibi na Mabwana

Habarini za Asubuhi

Awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Bi. Doris Mollel ambaye amechukua hatua ya kusaidia upatikanaji wa vifaa vya kusaidia watoto wachanga waliozaliwa na uzito mdogo pamoja na njiti kupitia taasisi yake ya kusaidia watoto waliozaliwa kabla ya siku zao(njiti), asante sana.

Utangulizi

Tanzania ni mojawapo ya nchi kumi zinazochangia kwa asilimia 66 ya jumla ya vifo vya watoto wachanga Duniani. Kipaumble cha afya ya jamii ni kupunguza vifo vya watoto wachanga chini ya umri mwaka mmoja mara tuu wanapozaliwa kwa sababu asilimia 29 ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano huchangiwa  na kundi hilo. Hivyo kuboresha maisha ya watoto wachanga ni muhimu katika kufikia malengo ya maendeleo ya Millennia pamoja na lengo Namba 3 la matokeo makubwa sasa linalohusu kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano. Katika muongo mmoja uliopita, Tanzania imejitahidi kupunguza vifo vya watoto wachanga. Jambo linaloleta faraja na matumaini katika kupatikana kwa njia bunifu na nia dhabiti ya kushughulikiatatizo hilo.

NchiniTanzania takwimu za Taifa zinazoonyeshwa kuwa asilimia 13 ya watoto huzaliwa wakiwa na uzito pungufu ambao huchangia kwa asilimia 86 ya vifo vya watoto wachanga. Uzito pungufu wa kuzaliwa una madhara makubwa na kuathiri uwezo wa watoto wachanga kuishi na kukua. Aidha kuzaliwa kabla ya muda ni tatizo linalochangia na kusababisha vifo vya watoto wachanga na inakadiriwa kuwa asilimia 27 ya vifo hivyo inasababisha madhara ya kuzaliwa kabla ya wakati.

Mipango na matunzo ya watoto wachanga kwa njia ya kangaroo kwa watoto wenye kuzaliwa kabla ya muda na wenye uzito pungufu ni mojawapo ya mikakati ya afya mtoto inayozingatiwa hali halisi na gharama nafuu ikitekelezwa katika eneo pana . Mpango huu hauhitaji nguvu kazi kubwa ikilinganishwa na mikakati ya kawaida ya matunzo ya afya ya mtoto ambao unahitaji rasilimari chache na hivyo na kuwa shughuli inayowezekanika kifedha na kiuchumi.

Kuanzishwa kwa Kitengo cha Watoto walioko kwenye Mafunzo ya Kangaroo

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ikishikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la Afya na Maendeleo ya Watoto (UNICEF), SAVE the Children waliandaa na kukubali mkakati wa matunzo haya ya mama kangaroo. Napenda kuwataarifu kuwampango huu umeonyesha mafanikio makubwa sana ya kuzuia vifo vya watoto waliozaliwa kabla ya siku na wenye uzito mdogo. Takwimu za Tanzania na pia katika hosptali yetu zinaonyesha kwamba, kati ya asilimia 20 mpaka 25% ya watoto wanaolazwa katika kitengo cha watoto wachanga ni kwa sababu ya kuzaliwa akiwa njiti au uzito mdogo.

Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuzingatia umuhimu wa mkakati wa kukupunguza vifo vya watoto  wachanga kama lengo la millenia namba 4 linavyoeleza  na pia kuzingatia dira na dhima ya Hospitali ya Taifa Muhimbili uongozi uliona umuhimu wa kuanzisha  kitengo cha Kangaroo ili kupunguza vifo vya watoto wachanga kwa gharama nafuu ili kufikia lengo la millenia la kupunguza vifo kwa asilimia 75% kufikia mwaka 2015.

Mwaka 2012 mwezi Agosti, kitengo hiki kilianzishwa kikiwa katika jingo la watoto kikiwa na vitanda nane, wauguzi 10, wahudumu wanne na madaktari wawili. Kwa sasa kitengo kinahudumiwa na madaktari wengi zaidi na idadi ya vitanda imeongezeka na kufika 30. Vilevile mwezi wa Julai mwaka huu, madaktari na baadhi ya waaguzi walipatiwa semina elekezi ya namna ya kuwahudumia watoto waliozaliwa njiti na uzito mdogo. Hii ilienda sambamba na upatikanaji wa mashine tatu za kusaidia kupumulia yaani bCPAP. Hivi vyote vimesaidia Zaidi kuboresha hali ya watoto wachanga wanaozaliwa na shida ya kupumua.

Takwimu:

Takwimu zetu za hospitali zinaonyesha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa vifo vya watoto wachanga. Katika mwaka 2012 kwa kila watoto 100 waliolazwa kulikuwa na vifo 25, na hali hii imepungua hadi vifo 16 kwa kila watoto 100 kwa mwaka 2014. Hii inatokana juhudi mbalimbali za serikali ikiwepo huduma ya kangaroo inayopatikana katika hospitali yetu.

Mafanikio kwa Watoto waliotunzwa kupitia njia ya Kangaroo

  1. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2012 mpaka mwaka2014 tumefanikiwa kuhudumia watoto wapatao 840. Idadi hii ni kubwa ikilinganishwa na vituo vingine ambavyo viko nchini.

 

  1. Kati ya vichanga hivyo tuliwahudumia watoto 837 sawa na asilimia 99.5% walioruhusiwa hai ikionyesha kwamba asilimia 0.1 ni sawa na watoto 3 waliofaliki katika kitengo hicho tangu Agosti 2012 hadi Disemba  2014.
  2. Kunyonyeshwa kwa watoto hao kuwa sehemu kubwa na faraja kwa akina mama wazazi na familia kwa wale wote ambao wamezaa kabla ya siku na watoto wenye uzito pungufu.

 

  1. Kupunguza msongamano wa watoto katika wodini ya watoto wachanga waliolazwa katika Hospitali Taifa Muhimbili kwenye chumba chenye incubator kwa asilimia kubwa.

 

Huduma zinatolewa kwenye Kitengo cha Kangaroo

  1. Usimamizi thabiti na utalaamu wa unyonyeshaji bora wa watoto wachanga (exclusive breast feeding)
  2. Usimamizi mzuri na wa uhakika wa kutunza joto la mwili na watoto hao kutunza joto la mwili (skin to skin contact).
  1. Tunahakikisha kwamba wameondoka na uzito uliokubalika kitaalamu kutokana na kufuatilia kwa karibu wale ambao wote wameruhusiwa katika kitengo cha mama kangaroo.
  1. Kuhakikisha wamepata chanjo zote dhidi ya adui maradhi yanayoshambulia watoto wachanga.
  1. Ufuatiliaji mkubwa kwa wale ambao wameendelea na matunzo nje ya mji wa Dar es salaam ikiambatana na mfumo mzuri wa ufuatiliaji (tracking system)  kwa kutumia simu (by phone referral system) mfumo mzuri wa kuwarifaa  kutoka kitengo hadi kitengo kingine kwa kutumia Sera za Hospitali na zile za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

 

Wito:

Tunatoa wito Kwa wizara ya Afya  Kuongeza vitengo vya kangaroo mpaka kwenye ngazi ya vituo vya afya kwani huduma hii ni muhimu sana kwa kupunguza vifo vya watoto wachanga na pia ni huduma ya gharama nafuu haihitaji utaalamu wa hali ya juu na vifaa Tiba vya gharama Kubwa. Vile vile kuwezesha upatikanaji wa vifaa tiba vya kisasa hasa katika hospitali yetu ya taifa ili kusaidia kuboresha huduma zakitaalum kwa watoto.

Aidha napenda kuwapongeza sana

Viongozi wenzangu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuzidi kuboresha huduma kwa watoto wanaozaliwa njiti pamoja na kukubali mpango wa uanzishwaji wa mafunzo hayo ya KMC. Nawapongeza wafanyakazi wote wa Jengo la Watoto na Jengo la Wazazi kwa ushirikiano wao katika kuokoa maisha ya watoto hawa.

 

Imetolewa na;

Prof. Lawrence Mseru

KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI

Novemba 17, 2015

Dar es Salaam, Tanzania. Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) leo Jumatatu Novemba 11, 2015, saa 06:00 mchana kutakuwa na mkutano na wana habari kuhusu maendeleo ya matengenezo ya mashine za CT- Scan na MRI .

Mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Bodi. Waandishi wa habari wanakaribishwa ili kuwajulisha wananchi maendeleo ya mashine hizo.

Mwanza, Tanzania. Watu 106 wamefariki dunia baada ya kuugua ugonjwa wa kipindupindu kutokana na ugonjwa huo kusambaa katika Wilaya 39 nchini.

Ofisa wa afya kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Maria Kitambi amesema kwamba ugonjwa huo umesambaa kwa kasi kutokana na wakazi wa maeneo husika kutozingatia usafi. Amesema kuwa ugonjwa huo umeenea kwa nguvu na kwamba Serikali inapambana kukabiliana na tatizo hilo.

Dar es Salaam, Tanzania. Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania wameipongeza Taasisi ya Kaimu Mkuu wa Taasisi Ya Moyo ya Jakaya Kikwete Mrisho iliyopo Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi akizungumza na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania kuhusu shughuli za upasuaji wa moyo zinazofanywa na taasisi hiyo.Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa kuanzisha huduma ya upasuaji wa moyo.

Mabalozi hao wamefurahishwa na huduma hiyo na kueleza kwamba watawashauri raia wao kwenda kupatiwa matibabu kwenye taasisi hiyo.

Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Balozi Edzai Chimonyo amesema kwamba wamefurahishwa na juhudi za taasisi hiyo na kwamba wanapenda kujua jinsi ya kuzuia matatizo ya moyo.

“Napenda kujua ni vipi mtu anaweza kuzuia matatizo ya moyo,” amesema Balozi Chimonyo.

Naye Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thami Mseleku amesema kwamba ataitumia taasisi hiyo kupima afya yake na kwamba endapo atatozwa fedha kwa ajili kupatiwa matibabu yupo tayari kutoa ili kusaidia wagonjwa wa kawaida wanaopatiwa matibabu hapo.

Akizungumza na mabalozi hao, Kaimu Mkuu wa taasisi hiyo, Profesa Mohamed Janabi amesema ili watu wasipate shinikizo la damu wanapaswa kufanya mazoezi, kupima afya mara kwa mara na kuchunguza endapo familia ina tatizo la shinikizo la damu.

Profesa Janabi amesema kwamba endamba mabalozi hao watazingatia hayo wataepuka kupata shinikizo la damu.

Awali Profesa Janabi amewaeleza mabalozi hao huduma zinazotolewa na taasisi hiyo ikiwamo kufanya upasuaji kwa watoto 37 hivi karibuni wakimo watoto wawili kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC).

Profesa Janabi amesema upasuaji wa moyo unaofanywa na hospitali hiyo unasaidia kupunguza gharama za matibabu endapo wangekwenda kutibiwa India.

Amesema gharama za mgonjwa kufanyiwa upasuaji wa moyo India ni kuanzia Dola 10,000 hadi 12,000 wakiwamo ndugu wanaomsindikiza mgonjwa nchini humo.

Dar, es Salaam, Tanzania. Wanafunzi waliosoma St. Joseph Cathedral High School zamani ikijulikana Sekondari ya Forodhani leo wamejitokeza kwa wingi katika shule hiyo kuchangia damu akiwamo Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Radhia Msuya.

Wanafunzi hao wa zamani wamekuwa kivutio kwa watu mbalimbali kutokana na ushirikiano wao katika kuokoa maisha ya wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

MNH imekuwa ikitoa matangazo mbalimbali ili Watanzania wajitokeze kuchangia damu kwa wagonjwa wanaopatiwa matibabu kwenye hospitali hiyo.

Katika shughuli ya leo, Balozi Msuya alifika katika shule hiyo na kuchangia damu kama walivyofanya wanafunzi wengine waliosoma hapo miaka 1950.

Balozi huyo alisoma katika shule hiyo mwaka 1975. Baadhi ya wanafunzi wengine ni Mariam Zialora ambaye amesoma hapo 1964, Glen Dias mwaka 1954, Saada Jaha mwaka 1970, Albertina Doarado mwaka 1968, Solomon Mihayo mwaka 1990, Tahir Othman 1990, Edith Mabena mwaka 1992, Edward Makwani mwaka 1970 na Ephrahim Tumwidike mwaka 2012.

Leo wanafunzi hao wa zamani wameonyesha upendo wa hali ya juu kuungana na wanafunzi wanaosoma kwenye shule hiyo hivi sasa katika kuchangia damu. Uamuzi huo wa wanafunzi hao wa zamani unapaswa kuigwa na shule nyingine kwa lengo la kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu.

Shughuli ya kuchangia damu leo imefanywa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS).

Rais Kikwete na Dk Slaa Wazindua Jengo la Bohari Kuu ya Dawa CCBRT

Dar es Salaam, Tanzania. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Rais wa Bodi ya Hospitali ya CCBRT ya jijini Dar es Salaam Dr Wilbroad Slaa alipokwenda hospitalini hapo kuzindua jengo la bohari kuu ya madawa katika hospitali hiyo. Kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe Seif S. Rashid na katikati yao ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salam Mhe Saidi Meck Sadick.Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa na Rais wa Bodi ya Hospitali ya CCBRT ya jijini Dar es salaam Dr Wilbroad Slaa kwa Mtendaji Mkuu wa CCBRT Bw. Erwin Telemans alipokwenda hospitalini hapo kuzindua jengo la bohari kuu ya madawa ya hospitali hiyo.Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali alipokwenda hospitalini hapo kuzindua jengo la bohari kuu ya madawa ya hospitali hiyo pamoja na mgahawa.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Bodi ya Hospitali ya CCBRT ya jijini Dar es salaam Dr Wilbroad Slaa na mabalozi na watoto wanaopata matibabu wakikata utepe kuzindua jengo la bohari kuu ya madawa ya hospitali hiyo pamoja na canteen. Kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe Seif S. RashidRais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua pazia kuashiria kufunguliwa jengo l bohari ya madawa huku akishuhudiwa na Rais wa Bodi ya Hospitali ya CCBRT ya jijini Dar es salaam Dr Wilbroad SlaaRais Kikwete akitembezwa katika bohari ya madawa ya hospitali ya CCBRT ambayo ni ya kisasa kabisa 
Rais Kikwete akitoa hotuba yake ya uzinduzi.


Rais Kikwete akitoa hotuba yake ya kuzindua majengo hayo


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa kwa hotuba na Rais wa Bodi ya Hospitali ya CCBRT ya jijini Dar es salaam Dr Wilbroad Slaa baada ya kuzindua jengo la bohari kuu ya madawa ya hospitali hiyo.

Page 1 of 4