Thursday, 05 September 2013 04:43

Magari ya Mizigo Yaliozuiliwa Mpakani Tanzania na Rwanda Yaruhusiwa

Written by 
Rate this item
(0 votes)

 

 

Magari Yaliozuliwa Mpakani Tanzania na Rwanda Yaruhusiwa

Zaidi ya magari ya mizigo 400 yaliyokuwa yamekwama katika eneo la Rusumo mpaka wa Tanzania na nchi ya Rwanda baada ya serikali ya Rwanda kupandisha kodi ya kutoka dola 152 hadi dola 500 kwa kila gari moja la mizigo hali hiyo imesababisha msongamano mkubwa mpakani.

Lakini kutokana na tozo hiyo mpya kusitishwa magari mengi yanapita Rwanda kwenda Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo .

Baadhi ya madereva wa magari ya mizigo wameiomba serikali ya Rwanda kufanya makubaliano na nchi wanachama wa Afrika Mashariki kwa kuwa na lugha moja ya kodi na kwamba malumbano yaliyopo kati ya rais wa nchi ya Rwanda na Tanzania na kwamba rais wa Rwanda amepandisha gharama bila taarifa kwa wasafirishaji na kusababisha usumbufu kwa madereva.

Kwa upandewake mmoja wa watendaji wa Serikali wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) katika eneo la mpaka wa Tanzania na nchi ya Rwanda Nasoro Ibrahimu amekili kuwapo kwa msongamano mkubwa wa magari ya mizigo katika eneo la Tanzania baada ya kuzuiliwa kuingia katika nchi ya Rwanda na kusababisha kufunga barabara ya rusumo ngara isipitike.

Read 709 times