Saturday, 15 September 2012 08:00

Ecobank yakabidhi zawadi za Sh10 milioni

Rate this item
(0 votes)

Watanzania wametakiwa kutumia huduma za benki ili wanufaike na mikopo pamoja na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki nchini.

Rai hiyo imetolewa leo  Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Ecobank Enoch Osei –Safo wakati akikabidhi  zawadi thenye thamani ya zaidi ya Sh10 milioni kwa washindi 15 wa shindano la shinda babu kubwa na Ecobenk.

Bosi huyo amesema Benki ya Ecobank nchini ni imeamua kutumia faida wanayoipata na wateja wake kwani hiyo ni njia nzuri wakuwanufaisha watanzania na kwamba njia sahii ya kuhifadhi fedha ni kuweka benki.

“Sisi tunawajali wateja wetu ndiyo mana tumeamua kutoa zawadi katika shindano ambalo tunaliendesha kutokana na jinsi wateja wetu wanavyo tumia huduma zetu jambo ambalo linatufanya tujumuike pamoja kwa kutumia faida tunayoipata.

“Benki yetu inawajali wateja wake ndio maana leo tunatoa zawadi zenye thamani ya Sh10 kwa wateja wetu 15 ambao wanatumia huduma zetu na kwamba katika hatua ya mwisho tutatoa gari lenye thamani ya Sh65 milioni,” amesema.

Benki hiyo imetoa zawadi ya Laptop, tiketi ya safari ya kwenda Zanzibar vocha ya manunuzi katika maduka mbalimbali yaliyoanishwa na benki hiyo pamoja Compyuta aina ya Ipad.

Naye Meneja wa Benki hiyo tawai la Mwenge  Patric Njole aliwapongeza washindi hao wa kuwataka watanzania kutumia huduma za benki katika shuhuli zao ilikupata faida na kufanya fedha zao ziwe salama.

 

Read 899 times Last modified on Saturday, 15 September 2012 08:48